Na Mayasa Mariwata
MAMA
wa msanii nguli wa filamu nchini marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa
amesema yuko katika mkakati wa kuandaa filamu inayohusu maisha ya
mwanaye kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msaada ‘kutembeza bakuli’.
Mama mzazi wa marehemu ‘Steven Kanumba’ Frola Mtegoa.
Akizungumza na paparazi wetu mama huyo alisema kwamba, anapata wakati
mgumu kukamilisha jambo hilo kutokana na kukwama na kutaka asaidiwe ili
kufanikisha jambo hilo.
“Nimekwama na nawaomba wadau wajitokeze kunisaidia nikamilishe hili, nahitaji msaada wa kifedha na hata ushauri,”alisema.
Mama
huyo alisema lengo la kuandaa kazi hiyo ni kutaka kufikisha ujumbe
katika jamii kwa kuamini kwamba wengi watajifunza kupitia maisha ya
mwanawe.
Marehemu Steven Kanumba.
Amemtaka yeyote ambaye atakayeguswa na jambo hilo asisite kuwasaliana naye na kumsaidia.