Stori: shakoor jongo na mayasa mariwata.
NDIYO habari ya ‘mujini’ kwa sasa, kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, mtangazaji wa kituo cha
runinga cha DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ wamemwagana, Risasi Jumamosi
limemwagiwa upupu.
Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ wakiwa pamoja katika pozi.
KAMA UTANI, WEMA ATAJWA
Kwa sharti la kutotajwa mahali popote, ‘mtonyaji’ wetu ambaye ni mtu wa
karibu wa wawili hao aliliambia gazeti hili kuwa chanzo cha Diamond na
Penny kuingia kwenye listi ya ‘zilipendwa’ kilianza kama utani.
Awali ilidaiwa kuwa kila mmoja amekuwa akijiona mwenye thamani mbele ya mwenzake huku Wema Sepetu naye akidaiwa kuwa chanzo.
Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
“Hakuna penzi tena kati yao, wameachana na kila mmoja yuko kivyake.
“Walianza kama utani, unajua wale kila mmoja anajiona yuko juu kuliko
mwenzake, lakini kitendo cha Diamond kuripotiwa kutoka na wanawake
tofauti mara kwa mara hasa Wema, kimemchosha Penny ndiyo maana ameamua
kujiweka pembeni kuepuka msongamano.
“Kupangwa kama mafungu ya nyanya inahusu?” alihoji ‘kikulacho’ huyo ambaye ni rafiki wa Diamond.
RISASI MZIGONI
Baada ya kutojiridhisha moja kwa moja na taarifa za awali kutoka kwa
rafiki huyo, timu ya gazeti hili kwa kuwatumia ‘wahangaikaji’ wake
maalum, iliingia mzigoni kupeleleza ukweli juu ya tetesi hizo.
Watu
kadhaa walio chini ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo rais wake ni
Diamond walihojiwa ambapo majibu yalikuwa yaleyale kwamba, kwa sasa
Diamond na Penny imebaki stori!
SHAKA ILIPOANZIA
Wakati timu yetu ikiendelea na uchunguzi wake makini juu ya uvumi huo,
hivi karibuni Diamond alionekana ‘singo’ kwenye pati ya kusherehekea
siku ya kuzaliwa ya ‘dada wa mjini’, Halima Haroun ‘ Halima Kimwana’
ambayo aliiandaa Diamond.
Minong’ono ya kuhoji kutoonekana kwa Penny
ilisikika ndani ya Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar
ilikofanyikia pati hiyo iliyojaa vitendo vya ufuska.
“Haiwezekani leo rais (Diamond) akajiachia peke yake bila Penny. Si kawaida ya Diamond.
“Kwa vyovyote watakuwa wameshamwagana kwa sababu kwenye pati zote huwa
wanakuwa pamoja tangu walipoanza uhusiano wa kimapenzi,” alisikika mmoja
wa waalikwa katika sherehe hiyo.
Katika tukio hilo, Penny alipigiwa simu na
paparazi wetu na kujibu kwa kifupi: “Naumwa. Halafu si lazima nije kwani
kila mtu ana ratiba zake.”
Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY KIZIMBANI TENA Baada ya kukamilisha
udadisi huo kupitia kwa watu wao wa karibu, gazeti hili lilianza na
Penny kwa kumuuliza undani juu ya habari hiyo lakini alionekana kuwa
‘mzito’ kwa kutoingia ndani kulizungumzia sakata hilo huku akiahidi
kulifungukia muda wowote kuanzia sasa.
“Kwa sasa sina cha kuzungumza
juu ya hilo, nitalizungumzia muda wowote tena si siku nyingi zijazo,
lakini si leo, tafadhali sana,” alijibu Penny kwa kifupi na sauti ya
chini iliyojaa uchovu.
Paparazi: “Hebu nisaidie, mko wote au hamko wote?”
Penny: “Nimesema sitoweza kusema lolote kwa leo, subirini.”
Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’. DIAMOND KIMYA
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu yake ya kiganjani, hakupokea
licha ya kupigiwa mara kadhaa kwa namba zake zote. Akatumiwa meseji
yenye maelezo yote, hakujibu.
MAMA DIAMOND
Ili kujiridhisha na madai hayo, waandishi wetu walimtafuta mama mzazi
wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye alisema hajui na hana taarifa
hizo.
NDUGU WA KARIBU SANA Baada ya mama Diamond, paparazi wetu alimpigia simu ndugu wa karibu sana na Diamond, sikiliza:
Paparazi: “Kumbe Diamond na Penny wamemwagana we huniambii. Sasa wifi yako mpya ni nani?”
Ndugu: “Aka! Sikwambii. Kwanza mi nipo mbali, sipo Dar.
WADAU WANAJUA
Haikuishia hapo, timu yetu ilizungumza na wadau mbalimbali ambao
walionesha kusikitika huku baadhi yao wakisema walitabiri tangu awali.
“Duh! Penny ameachia ngazi mwenyewe. Sisi tulijua hawawezi kufika
mbali, maana penzi lenyewe lilikuwa na mbwembwe nyingi,” alisema
mwanamke mmoja anayejua kila kitu.
TUJIKUMBUSHE
Siku za hivi karibuni Diamond alifanya mahojiano kwa njia ya mtandao
mmoja wa kijamii ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na
mpango wa kuoa ambapo alisema kuwa hana mpango huo kwa sasa na hatarajii
kumuoa yeyote kati ya wanawake wanaotajwa kwa sana midomoni mwa watu
(akiwemo Penny).
Wema alipigiwa simu juzi, lakini simu yake ilikuwa ikiita ‘weee’ mpaka inakatika, inaita ‘weee’ mpaka inakatika.