Kampuni ya Transevents Marketing Ltd
kutoka Nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious
Transport(DAT) linalotengeneza mabasi ambayo kutoka Uholanzi yanauwezo
wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya
kwanza kwa Afrika itakayo anzia Tanzania kuwa na aina hiyo ya
mabasi.
Mabasi hayo ya aina yake ambayo
yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa
mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza
foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha swala zima la usafiri ambapo
mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa
kupita majini na Nchi kavu.
Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu.
Mchakato huo umekwisha anza kufanyiwa kazi pia kwa ushirikiano wa SUMATRA
Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa
upembuzi yakinifu na kazi pia kwa ushirikiano na taasisi pamoja na
Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na
kitengo cha Usalama barabarani.
Video hizi Mbili zinaelezea kwa kina na kuonesha jinsi Mabasi haya yatakavyokuwa yakifanya kazi hapa nchini Tanzania