Stori: Issa Mnally
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa juzi Jumapili alitibuliwa na
waendesha pikipiki (Bodaboda) wa wilaya zote za jijini Dar Salaam
katika Viwanja wa Leaders baada ya kusukuma gari lake huku wakiimba
‘rais, rais, rais.’
Waendesha bodaboda wakisukuma gari la Lowassa huku wakiimba ‘rais, rais, rais.’
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli alionekana kutibuka alipopewa
nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo uliokuwa maalum kwa ajili ya
kuzindua saccos ya waendesha bodaboda ambapo alisema wanaomwita rais
wanataka kumkosanisha na watu.
Hata hivyo, hakusema anataka kukosanishwa na nani.
Lengo la
kuanzishwa kwa Saccos hiyo ni kuwasaidia waendesha bodaboda kujiongezea
kipato na kujinunulia pikipiki zao na kuachana na kuendesha pikipiki za
matajiri.
Edward Lowassa akiongea na waendesha bodaboda (hawapo pichani).
“Lengo langu mimi ni kutaka kuwaona mmejiajiri kwa kuendesha pikipiki
zenu wenyewe si za matajiri hivyo ni vizuri kuanzisha Saccos ambazo
zitawasaidia kujikwamua na kuendesha pikipiki za matajiri,” alisema
kiongozi huyo ambao walizidi kushangilia kwa nguvu ‘rais… rais..rais.’
“Jamani hizo kelele za rais, rais, mtanigombanisha yaani mnanichonganisha na watu,” alisema Lowassa.
Baada ya uzinduzi wa Saccos yao, Lowassa aliondoka viwanjani hapo huku
gari lake lilisukumwa na waendesha bodaboda hao ambao waliendelea kuimba
‘rais… rais’ na kuwapa kazi kubwa polisi ya kuwatawanya