Mashabiki wa timu ya Yanga SC.
Na Khadija Mngwai
SHIRIKISHO la
Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa kutokana na idadi ya mashabiki
waliozimia katika mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Yanga kuwa kubwa,
wameamua kuongeza magari ya wagonjwa ‘ambulance’ ikiwa ni sehemu ya
kushughulikia tatizo kama hilo endapo litajitokeza katika mechi ya kesho
baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.…
Mashabiki wa timu ya Yanga SC.
Na Khadija Mngwai
SHIRIKISHO la
Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa kutokana na idadi ya mashabiki
waliozimia katika mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Yanga kuwa kubwa,
wameamua kuongeza magari ya wagonjwa ‘ambulance’ ikiwa ni sehemu ya
kushughulikia tatizo kama hilo endapo litajitokeza katika mechi ya kesho
baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa timu ya Simba SC.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana katika mechi hiyo ya kirafiki ya
Nani Mtani Jembe ambapo katika mechi ya awali, watu zaidi ya 21
waliripotiwa kuzimia kwenye mchezo huo.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura amesema wameimarisha
ulinzi wa kutosha kwa ajili ya mchezo huo pamoja na kuongeza magari
hayo.
“Tutaongeza ambulance kutokana na hali iliyojitokeza katika
mechi iliyopita kwa kuhakikisha hakuna kitakachoharibika,” alisema
Wambura.