Diamond Platnumz akimmwagia manoti Halima Kimwana.
Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja KUFURU
ya kufunga mwaka! Dogo anayejua kuzitumia vyema fursa muhimu, Nasibu
Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefanya yake kwa mara nyingine, safari
hii amefanya pati iliyojaa ufuska, Ijumaa linaibumburua. …
Diamond Platnumz akimmwagia manoti Halima Kimwana.
Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja KUFURU ya
kufunga mwaka! Dogo anayejua kuzitumia vyema fursa muhimu, Nasibu Abdul
Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefanya yake kwa mara nyingine, safari hii
amefanya pati iliyojaa ufuska, Ijumaa linaibumburua.
Burudani zikitolewa na Kundi la Kibao Kata.
Msanii huyo kwa ‘kolabo’ ya swahiba wake mkuu ndani ya anga la muziki
Bongo, Omari Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ alifanya tukio hilo lililoacha
watu midomo wazi mwanzoni mwa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Business Park
uliopo Kijitonyama, Dar.
Pati hiyo ilikuwa ya kumpongeza mtu wake wa karibu katika Wasafi Classic Baby (WCB), Halima Haroun ‘Halima Kimwana’.
Halima Kimwana akionyesha baadhi ya manoti aliyotunzwa.
FUNUNU ZA PATI Ngoma za masikio ya ‘viranja’
wetu yalinasa fununu za kuwepo kwa kufuru hiyo mapema mwishoni mwa wiki
iliyopita na kuanza kuandaa ‘patroo’ maalumu ili kunasa matukio muhimu.
SIKIA FUNUNU ZENYEWE Akizungumza na waandishi
wetu kwa usiri na sauti ya ‘kimbeya’, mmoja wa rafiki wa Diamond (jina
kapuni) aliweka wazi kwamba Diamond alipania kumfanyia Halima pati hiyo
ikiwa ni moja ya matukio yatakayoendelea kukumbukwa kwa mwaka huu.
Mmoja wa wasanii wa Kundi la Kibao Kata akifanya vitu vyake.
“Diamond amepania kufanya makubwa kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa ya
Halima ikiwa ni moja ya matukio yake muhimu yatakayokumbukwa. Itakuwa ni
pati ya kufa mtu,” alisema ‘kikulacho’ huyo.
MAANDALIZI Duru za habari zilizidi kudai kuwa,
maandalizi ya sherehe hiyo yaliingiliwa kati na Diamond na kumzuia
Halima asitumie fedha zake na kwamba kila kitu na gharama zote za juu
zitakuwa juu yake.
Steve Nyerere naye akitoa 'misimbazi' kwa Halima.
SIKIA HII Katika moja ya maandalizi ya sherehe
hiyo, walialikwa wacheza shoo maalumu ‘Kibao Kata’ wakiwemo wake za watu
ambao siku hiyo walifanya ‘usodoma’ uliomfanya hata shetani mwenyewe
afumbe macho kwa aibu.
SIKU YA SIKU Hatimaye siku ya sherehe hiyo
iliwadia Jumatatu ya wiki hii, mastaa muhimu wa mrembo huyo wakaalikwa.
Ngoma ya Kibao Kata na muziki wakalamba 500,000, ikawa ni mwendo wa
kumwaga lazi kwa kwenda mbele.
...Mambo ya kumwaga radhi hayo.
MASTAA Weka mbali Diamond aliyekuwa ‘mwenyeji’
wa sherehe hiyo, wasanii wengine waliodondokewa na bahati ya kuhudhuria
pati hiyo iliyotawaliwa na matukio machafu ni pamoja na Nurdin Bilal
‘Shetta’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Juma Said ‘Chegge
Chigunda’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, Ommy Dimpoz, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’ , Husna Maulid na wengine kibao.
Diamond na Ommy Dimpoz (kulia) wakipata msosi katika 'bethidei' hiyo. Kushoto nyuma ni msanii Shetta.
Katika sherehe hiyo ambayo Halima Kimwana alitimiza miaka kadhaa
tangu aanze kuvuta hewa ya oksijeni, muziki wa ladha mbalimbali
ulitawala huku nyimbo za ‘kaka mdogo‘ huyo zikichosha ngoma za masikio
ya wahudhuriaji.
‘MISIMBAZI’ YATAWALA Ili neno historia litimie,
Diamond alifungua ukurasa wa kumwagia Halima ‘mvua’ ya noti nyingi za
shilingi elfu kumikumi zilizokadiriwa kuwa Sh. milioni moja na ushee.
Misimbazi iliyokusanywa katika sherehe hiyo.
Mbali na Diamond, Ommy Dimpoz alijibu mapigo kwa kumimina kiasi
kikubwa cha ‘misimbazi’ ambayo ilikaribiana na ile aliyomwaga swahiba
yake.
Hata hivyo, wasanii wengine hawakurudi nyuma ambapo walitoa kiasi
kikubwa cha fedha na kumfanya Halima kuelemewa na mzigo wa noti nyekundu
zilizokaribia shilingi milioni nne.
Burudani zikiwa zimepamba moto.
KISA NA SIRI Inadaiwa kuwa, kisa cha Diamond
kuamua kumfanyia sherehe hiyo Halima, ni moja ya zawadi ya kumtunzia
kumbukumbu muhimu za nyimbo zake mpya.
...Huyu akionyesha manjonjo yake juu ya meza.
“Unajua Halima amekuwa akimpa Diamond sapoti kubwa kwenye suala la muziki wake.
“Pia Halima ni mmoja wa memba wa WCB kwa hiyo ilikuwa lazima Diamond
kama rais wao amfanyie sherehe ya kufuru,” alisema mmoja wa watu wao wa
karibu.
Halima akimlisha keki Chegge.
HALIMA KIMWANA ACHEKELEA Waandishi wetu walianza kazi yao kwa kumbana Halima azungumzie ishu hiyo ambapo alisema:
“Nilisikia furaha sana na niliamini kweli Diamond ananipenda na
kunithamini. Aliwahi kuniambia kuwa siku yangu ya kuzaliwa atanifanyia
pati lakini sikuamini kwani huwa ananitania sana, ikawa sapraizi
kwangu.”
Queen Darleen akichukua baadhi ya matukio.
BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND ‘Mashushushu’ wetu
waliendelea na upekepeke wao ili kujua undani zaidi ambapo Diamond
alikiri kufanya hivyo na kuthibitisha madai ya kuwa ilikuwa ni zawadi
maalumu.
“Watu wengi hawajui ukaribu wangu na Halima una faida gani,
ukweli ni kwamba yule ni zaidi ya dada yangu, tumetoka mbali na amekuwa
akinisaidia katika mengi ya kisanii,”alisema.
Halima akipozi na msanii Nay wa Mitego.
KUHUSU UFUSKA “Jamani, ile ilikuwa sherehe sasa utawazuia watu wasicheze kweli? Ni kawaida kabisa, walikuwa na furaha,” alisema Diamond.
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA Licha ya gazeti hili
kumpongeza Diamond na Ommy Dimpoz kwa kuthamini michango ya watu wao wa
karibu, linakemea vitendo vya kifuska ambavyo vimekuwa vikifanyika
kwenye sherehe mbalimbali za mastaa kwani ni kinyume na utamaduni wetu.