
Rapper maarufu duniani Shawn Carter "Jay Z" akishirikiana na Cohiba Red
Dot wameamua kuanzisha biashara ya Sigara, sigara hiyo ambayo imepewa
jina la "
Comador" ikiwa ni Cigar
yenye kiwango na ubora wa hali ya juu. Imegharimu miaka miwili katika
utengenezaji wa Cigar hiyo mpaka kufikia kutumika ikiwa ni pamoja na
kutafuta tumbaku inayofaa kwa ajili ya bidhaa hiyo mpya.
Hii ni hatua kubwa kwa Star huyu katika kupanua uchumi wake, pia tunaona
hata kwa wasanii wengine nchini Marekani kama P.Diddy ambae nae ana
biashara zake ikiwemo kinywaji chake cha Ciroc Vodka na kimekubalika
sana katika soko.
Waweza tembelea website ya bidhaa hii mpya ili kujua mengi zaidi -
http://www.comadorcigar.com