
Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva,
Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari
ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.
Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia
mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond
Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea
ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi
hata show ya milioni 7. Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru
kwa sababu rekodi ninayo."
Nimeongelea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa
ndio wanaonekana kuongoza. Hata katika mambo yenu ya kumi bora za
Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya.
“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona
mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana.
Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na
watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.
“ Kwa sababu Diamond wa mwaka 2010,2011,2012 ni Diamond aliyekuwa
anapiga show Mlimani City sehemu alipozaliwa Dar es Salaam kwa kiingilio
cha shilingi 50,000, siku tatu kabla ya tukio tiketi zimekwisha. Kwa
hiyo Diamond wa hivi sasa ni yule ambaye anapiga show Tabora sehemu
ambayo hajawahi kuonekana, kwa kiingilio cha shilingi 5,000 na watu
hawaingii na bado walioingia wanampiga mayai viza na mawe.” Ametoa
mchanganuo wake.
Mtu huyo akafika mbali na kuapa, “ amini, sitakufa kabla haki hii
haijatendeka, naapa…kwa heshima ya mwenyezi Mungu aliyeniumba. Anasema
pigania chako ali hali hata ukifa ili mradi ulikuwa unapigania chako.”
Hata hivyo, Naseeb Abdul aka Diamond aliwahi kumkana Dr. Yahya na kueleza kuwa hamfahamu na hajawahi kumuona.