Lori
la mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T772 BAZ
limetumbukiakwenye mtaro eneo la Kihonda barabara kuu ya Morogoro Dodoma
baada ya dereva wa Lori hilo kushuka na kuliacha gari hilo bila
kulizima na kuwafukuza wezi waliokuwa juu ya tenk la gari hilo
wakishusha mizigo.
"
Dereva wa Lori hili alipofika pele kwenye tuta alishuhudia pikipiki
ikiwasha taa na kuzima aliamua kuongeza umakini na kubani kwamba mmoja
wa abiri aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo alipanda juu ya Tenk na kushusha
maboksi ya Oil ndipo dereva huyo aliposhuka akajisahau kuvuta
'endbrack'hivyo wakati akiwafukuza wezi hao huku Lori hilo lililokuwa
kwenye mtelemko lilitembea bila dereva na kuingia kwenye mtaro
Dereva
wa Lori hilo Bw ldd Hoza alipohojiwa alisema alikuwa akisafirisha
mafuta ya petroli kutoka Dar es salaama kueleka Dodoma na kwamba
alipofika kwenye daraja la Kihonda alipunguza mwendo kwa lengo la
kulipanda tuta lililokuwa eneo hilo la daraja.