Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake Dkt.Christina Ishengoma amesema katika kipindi cha mwaka 2013
wananchi wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakifanyakazi kwa kujituma na kwa
ushirikiano mkubwa.
Kwa upande mwingine ishengoma amewataka wananchi wote wa mkoa wa
iringa kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa kupanda mazao
yanayovumilia ukame ambayo ni Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na Ulezi kwa
na kila familia ihakikishe inapanda chini ya hekari mbili.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutawahakikishia uhakika wa chakula
hasa maeneo ambayo hupata mvua chache. Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo
amewaasa wananchi kutumia mbegu bora za kilimo,mbolea ya kundia na
kukuzia hasa kwa mazao ya mahindi na mpunga ili kupata mazao bora.
Aidha Ishengoma amewatakia heri ya krismasi na mwaka mpya huku
akiwahakikishia kuimalishwa kwa ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu.