Stori: MWANDISHI WETU DUNIA
ina mambo jamani! Mfanyabiashara wa madini aliyefahamika kwa jina moja
la Jimmy amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufumaniwa na mkewe
akiwa na kimada gesti.
Tukio hilo lililofunga mtaa kwa kujaza wambea kibao, lilitokea hivi
karibuni ndani ya gesti hiyo (jina tunalo) Kinondoni jijini Dar es
salaam ambapo mke wa mfanyabiashara huyo (jina halikupatikana mara
moja), alimnasa mumewe akijiandaa kuvunja amri ya sita ya Muumba.
Mke wa mfanyaiashara (kulia) baada ya kumfumania kimada akiwa na mumewe gesti maeneo ya Kinondoni, jijini Dar.
Wadakuzi waliokuwa eneo la balaa walitonya kuwa, siku hiyo ya tukio,
Jimmy ambaye ni mkazi wa jijini Arusha, alifika Dar kibiashara na
baadaye alimsaka kimada huyo wa siku nyingi na kwenda kujirusha naye
bila kujua mkewe alishatonywa juu ya usaliti wake.
Awali chanzo makini kinachojua nini maana ya habari kiliwatonya
mapaparazi wetu mara baada ya kupata mchongo wa fumanizi kutokea Sinza
ya Kumekucha lililoandaliwa na mke wa Jimmy.
“Nyie njooni tu hapa Sinza-Kumekucha ndipo mkewe alipotonywa na
dereva wa mumewe kuwa anaibiwa na kimada. Kuna gesti moja ipo ndani
kidogo upande wa kushoto kama unaelekea Shekilango,” kilisema chanzo.
Timu ya mapaparazi ilifika katika gesti hiyo lakini bahati mbaya
waliambiwa kuwa, Jimmy na kimada huyo walihamisha kiwanja cha starehe na
kwenda Kinondoni.
Kimada aliyefumaniwa na mume wa mtu.
Mapaparazi walipofika katika gesti hiyo ya Kinondoni, walimkuta mke
wa Jimmy hivyo wakaambatana naye pamoja na askari polisi wawili kwa
ajili ya kwenda kufumania.
Jimmy kabla ya kuingia gesti inadaiwa
alijipumzisha katika grosari iliyo karibu na Mango Garden Bar, baadaye
akaenda kwenye gesti hiyo ya jirani bila kujua mkewe alikuwa akitua mguu
kila pale yeye aliponyanyua, akazama ndani ya gesti hiyo na kuanza
kujiandaa kwa zinaa.
Mke wa Jimmy hakuwa mbali, baada ya kujiridhisha mumewe amezama
chumbani, dakika kadhaa na yeye alitokea na kugonga mlango wa chumba
hicho kufuatia kutonywa na mhudumu mmoja wa gesti hiyo.
Jimmy alikutwa tayari ameshavua nguo zote na kubakiwa na ‘boksa’ huku kimada naye akiwa na ‘kufuli’ pekee.
Kilichofuata hapo ni kipigo, mke wa Jimmy alianza kumtembezea kipigo
yule kimada. Mapaparazi walivamia na kutandika picha za timbwili ambapo
Jimmy alifanikiwa kupenya mlangoni na kukimbia bila kujali nguo
nyingine.
Kutokana na kelele za timbwili hilo, majirani wa eneo hilo
walifika kuhoji kulikoni ambapo mfumaniaji huyo alitoboa siri kwamba
amekuwa akimfuatilia mumewe kwa siku nyingi baada ya kuambiwa ana kimada
Dar.
“Huyo malaya akome kutembea na waume za watu. Nimekuwa nikimfuatilia
mume wangu kwa muda mrefu. Nimetoka Arusha mpaka Dar kwa ajili yake.
Kweli za mwizi ni arobaini, leo nimewanasa,” alisema mwanamke huyo huku
akiondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana.
Wakati pakichimbika, kimada huyo alisikika akimlaumu Jimmy kwamba
amemuingiza kwenye mkenge akijua mkewe ni mdodosaji wa mambo na anaweza
kufika Dar madai ambayo hayakuwa na wa kuyajibu.
Taarifa zaidi zilidai kuwa ndugu mmoja wa mwanamke huyo ndiye
aliyekuwa na mchoro mzima wa Jimmy na hivyo ‘kuuza’ kwa mwanamke huyo.