Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiwapa mafunzo wahudumu wa
kituo cha mafuta cha OilCom kilichpo katika makutano ya barabara ya
Libya na Morogoro jijini Dar es salaam juu ya namna ya wateja wanaojaza
mafuta kituoni hapo wanavyoweza kulipia kwa njia ya M-pesa. Huduma ya
malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya OilCom vya TMJ
Msasani na Kipawa.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimjulisha Mahmud…
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiwapa mafunzo wahudumu wa
kituo cha mafuta cha OilCom kilichpo katika makutano ya barabara ya
Libya na Morogoro jijini Dar es salaam juu ya namna ya wateja wanaojaza
mafuta kituoni hapo wanavyoweza kulipia kwa njia ya M-pesa. Huduma ya
malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya OilCom vya TMJ
Msasani na Kipawa.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimjulisha Mahmud
Mohamed aliyefika kujaza mafuta kwenye kituo cha OilCom kilichopo kwenye
makutano ya barabara ya Libya na Morogoro jijini Dra es salaam kuhusu
kuwepo kwa huduma ya malipo kwa njia ya M-pesa kituoni hapo. Kushoto ni
Meneja wa IT wa kampuni hiyo ya mafuta Abubakar Mohammed. Huduma ya
malipo kwa M-pesa inapatikana pia kwenye vituo vya OilCom vya TMJ
Msasani na Kipawa.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiongea na Mteja wa
OilCom Esmail Abdulrahaman kuhusu kuzinduliwa kwa huduma ya malipo kwa
M-pesa kwenye vituo vya OilCom Msasani TMJ, Makutano ya barabara ya
Libya na Morogoro na Kipawa jijini Dar es salaam. Kulia ni mtumishi wa
OilCom Ala Mohammed.
Meneja wa IT wa Kampuni ya OilCom Abubakar Mohammed akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa kituo cha
OilCom kilichopo kwenye makutano ya Barabara ya Libya na
Morogoro.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na
kulia ni Meneja Msaidizi wa kituo hicho Hussein Ahmed.
Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
VODACOM YATOA MAFUNZO NAMNA YA KULIPIA MAFUTA KWA M PESA
Dar es Salaam Desemba 15, 2013 …
Kampuni ya mawasiliano ya simu, Vodacom Tanzania leo imeendesha mafunzo
kwa watumishi wa kituo cha mafuta cha OilCom kilichopo kwenye makutano
ya barabara ya Libya na Morogoro kuhusu huduma ya kulipia kwa njia ya
M-pesa.
M-pesa na OilCom walizindua huduma
inayowawezesha wateja wao kulipia kwa njia ya M-pesa wanapopata huduma
kwenye vituo vya OilCom vya TMJ Msasani, Kipawa na Libya.
“Tunawapatia
mafunzo wateja na watumishi kwenye vituo hivi ili kila mmoja aweze
kunufuika na kile tunachowapatia kupitia M-pesa. Tunafurahi kuona huduma
hii imepokelewa vizuri na inatumika bila ya shida yoyote.”Alisema
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom, Salum Mwalim.
“Lengo letu kuu ni kujua mandeleo ya huduma
yetu ni jinsi gani inatumika hapa, tumekuja kupata maoni ya wauzaji
pamoja na wateja wao pia kuwaelekeza pale wanapokwama. Hatutaki yale
tuliyokubaliana siku ya ubia yaishie kwenye vyombo vya habari, tunataka
kupata maoni ya wateja wetu moja kwa moja ili tuwasaidie.” Alisema Salum
Salum aliongeze kuwa kutembelea
kunawasaidia sana wateja wao na hata kuwaondelea wasiwasi juu ya huduma
ya M-Pesa na kwamba watafanya hivyo kwenye vituo vyote vya OilCom ambapo
huduma ya M-pesa inapatikana.
Akizungumza kituoni hapo Meneja wa IT
wa kampuni ya OiCom Abubakar Mohamed amesema huduma hiyo iliyozinduliwa
wiki tatu zilizopita yayari imeshakubalika kwa wateja na kwamba
wameifurahia kw akuwa inawaondolea usumbufu wateja wao.
Tumefurahi sana na inakwenda vizuri.
Mipango inaendelea kuahkikisha vituo vyote vya OilCom vya jijini Dar es
salaam vinawezeshwa kufanya malipo kwa njia ya M-pesa.”Alisema
Amesema
wateja wateja wa OilCom hawana sababu yoyote ya kutoitumia njia ya
M-pesa kufanya malipo kwenye vituo ambavyo tayari vimeshawezeshwa na
kwamba kampuni yake imejiapnga kisawasawa kuendelea kutoa huduma bora
kwa wateja wake.
Esmail Abdulrahaman ni mmoja wa wateja
waliofika kujaza mafuta kituoni hapo, kwa upande wake yeye amesema
“Huduma hii ini nzuri na inaleta urahisi sana ni vema tunajua uwepo wake
na hakuna shak inatushaiwhsi kuitumia ili kuondoa usmbufu na utegemezi
kwenye njia moja tu ya malipo ya fedha taslimu.”
Kwa upande wake Mahmud Mohammed lisema kuwa
yeye ni mteja mzuri sana wa mafuta ya kituo cha Oilcom na kudhihirisha
kuwa huduma hii imemletea faraja kubwa sana kwani kwa sasa hatokuwa
akibeba fedha nyingi badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa
na kufanya mizunguko yake akiwa na uhakika kwa kuweka mafuta kwenye gari
lake.
Hivi karibuni kampuni ya Vodacom Tanzania
na Oilcom ziliingia ubia ambapo wateja wa pande zote mbili wamewezeshwa
kulipia mafuta kwa kupitia huduma ya M-Pesa popote kwenye vituo vya
kampuni hiyo ya mafuta. Kwa kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar
es Salaam na kituo cha mafuta cha TMJ Msasani kikiwa cha kwanza
kuunganishwa na huduma hiyo huku vingine viwili vimefatia kisha huduma
hiyo kusambaa nchi nzima palipo na huduma ya M-Pesa na vituo vya mafuta
vya Oilcom.