Hadi jana Ijumaa, Justine Sacco, alikuwa afisa wa juu wa PR kwenye kampuni ya InterActiveCorp, yenye makazi yake New York inayomilikiwa na Barry Diller.
IAC inamiliki mitandao ya Daily Beast, Vimeo, About.com, Match.com, Ask.com, na mingine.
Kwenye akaunti yake ya Twitter ambayo tayari imefutwa, anajielezea kama “troublemaker on the side” known for her “loud laugh.” Si jambo la kushangaza wajihi wake huo kumfanya afanye hiki alichokifanya sasa.
Jana alitweet kitu cha kijinga kilichowafanya watu wajiulize kama akaunti yake imekuwa hacked ama alidhamiria kweli.
‘Going to Africa. Hope I don’t get AIDS. Just kidding. I’m white!
‘Naenda Afrika. Naamini sitapata Ukimwi. Natania. Mimi ni Mzungu’
Hakuna aliyejua kuwa akaunti ya Justine Sacco ilikuwa hacked, ama aliacha simu yake alipopanda ndege jijini London. Lakini hiyo haikufanya IAC kutolaani kitendo hicho:
“This is an outrageous, offensive comment that does not reflect the views and values of IAC. This is a very serious matter and we are taking appropriate action”
Kufuatia tweet yake hiyo, tayari kumeanzishwa hashtag iitwayo #HasJustineLandedYet.