Mimi
ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu
maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kuniangamiza maana
nimeshawaangamiza wengi sana kwa UKIMWI ila mengine yote usifute hata
moja ili dunia ijue tu japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi nilionao.
Nilizaliwa
mkoa wa Dodoma na nilishi vizuri tu tangu utotoni na hata sikujihusisha
na ngono hadi nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada ya kumaliza nilikuja
hapa Dar kuishi kwa mama mdogo aliyeolewa hapa Mwenge.
Nilipata
marafiki wengi tu na kuna kijana mmoja alinitongoza kwa muda mrefu sana
na siunajua vijana wengi hutumia muda mrefu kutongoza ili msichana
unadhani kwamba labda huyo anakupenda kumbe anataka tu ngono na wadada
wengi sana hudhani kufuatiliwa kwa muda mrefu na mvulana basi huyo yuko
serious kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila
nilikataa kuhusu kufanya mapenzi maana anayekupenda kiukweli sio uongo
lazima asitake ngono kabla ya ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6
aliniambia kuhusu kufanya mapenzi nilikataa alitumia mbinu nyingi sana
kwa kunibembeleza na hata kulia mbele yangu ili tufanye tu mara moja ila
nilikataa, alisema atavumilia hadi siku ya ndoa yetu ambapo tulipanga
kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye kumbi
za starehe na mimi kwa sababu ya upagani na kumwamini pia kwa sababu
nampenda nilikubali tulienda huko na kulikua na bendi fulani maarufu ya
mziki wa dansi ilikua inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na
mpenzi wangu akaagiza pombe alianza kunywa huku akinionjesha, nilikataa
kwa sababu nilikua sijawahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, hata
sijui alinishawishi vipi nilijikuta nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa
tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5 nadhani nikunywa kama bia 3 au 4
japokua nilikua nakunywa kidogo kidogo tu tena kwa kunywesha na mpenzi
wangu maana nikama nikua nanyweshwa kila baada kama ya dakika 25 ndipo
nakunywa mara moja na sikujuia kama nakunywa pombe ila niliihisi tu
naonja ili kumlizisha mpenzi wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri
nilihisi usingizi na pia nilijiona wa tofauti najua nililewa hata kama
sikujua kama nimelewa maana nakumbuka tulitoka pale huku amenishika
mkono huyo mpenzi wangu. Tulikodo tax na kuondoka na siku hiyo
aliniambia twende kwake alikokua amepanga chumba maana tulikua na
usingizi sana nilikubali huku nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika
salama na kuingia ndani ukweli pombe ni kichocheo cha ngono na ningekua
mimi ndio Raisi wa Tanzania ningefunga bar zote. Nilijikuta natamani
kufanya mapenzi na huyu mpenzi wangu hata alikua hana nia maana alijua
atanichukiza sana na uhusiano ungekufa siku hiyo lakini kwa sababu ya
pombe nilimwambia siku hiyo tufanye kidogo maana mwili wangu unataka.
Ni
kweli siku hiyo kwa sababu ya pombe nilifanya mapenzi na huyo mpenzi
wangu na baadae akanipeleka nyumbani baada ya wiki mbili maana tulikaa
wiki mbili bila kuonana alikuja na kunieleza habari ambayo sikuihitaji
katika maisha yangu maana nilikua nasikia tu kwa watu wengine lakini sio
kwangu alisema ”JANE ISHI KWA MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano iliyopita na anapenda tu ngono maana hawezi kuacha.
Nililia
sana na baada ya wiki moja baadae nikaenda kupima na kukutwa nina
ugojwa ambao niliusikia tu kwa watu na chanzo cha yote ni pombe, kupenda
starehe,disko na upagani unaotusumbua wanadamu wengi.
Nilikua na
UKIMWI na kwa hasira maana mpenzi wangu alihamia Arusha huku akisema
neno moja la mwisho kwamba ”shetani amemtuma kuwaambukiza wanadamu
UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua, sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh
YESU nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa mzigo ambao haukunistahili mimi.
Hata leo hua najiuliza kwamba nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini pombe
na huyu wakala wa shetani wamenifanyia hivi. Baada ya kujua nina UKIMWI
na hali hiyo nikaikubali na kulikua na kundi kubwa sana la wanaume
ambao walikua wamewahi kunitongoja na niliwakataa sana kwa sababu hii
niliwakubali ili nami nife na wengi.
Nilianza kumkubali kila
mmoja na kuna baba mmoja ambaye ana wake 3 niliwahi kumtukana sana
kipindi cha nyuma kila aliponitongoza lakini wakati huu nilimkubali na
hakuamini na tukafanya ngono tena bila kinga na akaniaachia pesa laki 6
kama zawadi ya kumkubali kumbe naye hakujua kuwa namwambukiza na hata
leo hua nawahurumia tu wale wake zake ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu.
Kiukweli
tangu may 2009 hadi 2012 nimeshatembea na wanaume zaidi 1500 maana
ilifika kipindi nala na wanaume 3 kwa siku na lengo langu niwakomeshe
kama mimi nilivyokomeshwa na nina uhakika kutokana na mimi wameambukizwa
UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa
linaniliza kila siku maana hata mimi najua kabisa nilianzisha mtandao
kama huo wa ngono kwa idadi kubwa sana ya watu.
Nimeokoka miezi 7
iliyopita na siku naombewa nilikutwa na mapepo mengi sana na hata
waombeaji wakashangaa. Ningejua ningeokoka tangu nikiwa na miaka 5
lakini ndio hivyo sina jinsi wala uwezo wa kubadirisha hali hiyo.
Na
naomba kila atakayesoma ujumbe huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni
dhambi pia kwenda disko ni dhambi,kuuza pombe ni dhambi na kila
kichochoe chochote cha dhambi ni dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi
kujua kama nina UKIMWI na sijui MUNGU ana mpango gani na mimi maana
kwake yote yanawezekana. Nauamini uponyaji wake na sijawahi kutumia ARV
hata siku moja na afya yangu iko sawa tu na huwezi hata wewe kujua kama
uovu huu nimefanya mimi.
Ndugu zangu kama una UKIMWI nenda
kanisani ukaombewe na kama una akili mpe YESU maisha yako maana pia
baada ya kifo ni hukumu. Yasalimishe maisha yako kwa YESU na usiambukize
wengine tena.
Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya mapenzi tena
na sitafanya hivyo wala sitaolewa na mtu yeyote maana yatosha kwa uovu
niliofanya na hadi sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15 wameshafariki na
nilihudhulia misibani huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.
Mwisho
nawashauli wababa kulidhika na wake zao na wamama pia lidhikeni na waume
zenu, vijana ambao hamjaoa wala kuolewa subiri hadi utakapooa au
kuolewa na kabla ya kuolewa au kuoa kapimeni kwanza kwani wenye UKIMWI
ni wengi kuliko unavyozani.
Fuata unachofundishwa kanisani na pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki
Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania.
Title : "NIMEAMBUKIZA UKIMWI MAELFU YA WATU JIJINI DAR"..JANE WA MWENGE DAR AFUNGUKA..SOMA ZAIDI HAPA
Description : Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es salaam naomba utalifuta jina la baba yangu maana sitaki liwe kwenye blog watu watanijua na kunianga...
Rating : 5