Muimbaji wa ‘Kitu Kimoja’ na ‘Hakuna Yule’, mrembo Avril Nyambura hayupo tena sokoni.
Kwa mujibu wa mtandao wa Standard Digital Entertainment, Avril
amechumbiwa na raia wa Afrika Kusini aishiye jijini Nairobi na wamepanga
kufunga ndoa mwakani.
“Hatimaye nina mwanaume. Tumekuwa pamoja kwa muda na nampenda sana,” alisema Avril. “Ni mtu wa Afrika Kusini,” aliongeza.