MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa
kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid
Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na
kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata
bahati ya kuolewa naye.
“Unapofika
umri fulani suala la kuolewa si mjadala bali ni lazima iwe hivyo lakini
shida inakuja je utaolewa na mwanaume anayekujali, kuheshimu na
kukupenda? Basi kwangu nataka kuolewa na mwanaume kama Kingwendu naamini
nitakuwa na amani raha mstarehe, tofauti na kama nitapata sharobaro
sina hakika kama atanijali,”anasema Rayuu kwa fulaha.
Rayuu alisema hayo alipoongea na Maskani Bongo katika mahojiano yake
na gazeti hili kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na
kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia
sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni
msanii mwenzake Kingwendu au anayefanana naye.