Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni,
Zakaria Kimemeneki (kulia), akikabidhi zawadi ya picha ya Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa
Dar es Salaam, Mohamed Cholage, wakati wa kufungwa semina ya Baraza la
UVCCM kata hiyo, jana. Picha hiyo imetolewa na UVCCM Mabibo, ili
akabidhiwe Nape kutokana na kutambua mchango wake katika kuijenga CCM.
Zaidi ya Vijana Wajumbe 30 walishiriki semina hiyo.
Mwenyekiti
wa UVCCM akakabidhi picha ya Kamanda wa UVCCM Kata ya Mabibo, Dk.
Fenella Mukangara ili nayo imfikie kwa kushukuru mchango wake kwa kuilea
jumuiya hiyo.
Mwenyekiti
huyo wa UVCCM akimvalisha Cholage kofia maalum ambayo UVCCM hao
wanasema walimuona kwa mara ya kwanza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman
Kinana ameivaa baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma.
Cholage
akitoa kitabu cha Kanuni za UVCCM kwa mmoja wa washiriki wa semina
hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabibo, Bononi Mlowe.
Wanasemina wakimsikiliza mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akivishwa skafu baada ya kuwasili kwenye ukumbi. Alisema hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuvishwa skafu!!